Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nani Amechukua Maski Yangu Jameni? Rais Aonekana Mkali Wakati wa Mkutano Ikulu

E6cbd6070c3a9d0d Nani Amechukua Maski Yangu Jameni? Rais Aonekana Mkali Wakati wa Mkutano Ikulu

Sat, 27 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Rais aliskika akiguruma kama simba baada ya kusahau alipokuwa ameiweka maski yake wakati wa kutoa hotuba kwa taifa

- Mawaziri wake waliingiwa na wasiwasi huku wakitafuta maski ya mdosi ilipokuwa imeenda

- Ni video ambayo inaonyesha mambo ambayo huwafanyikia walio karibu na Rais wakati mwingine

Mawaziri walioandamana na Rais Uhuru Kenyatta wakati wa kuhutubia taifa kuhusu hatua mpya za kupigana na Covid-19 waliingiwa na wasiwasi kwa muda baada ya mdosi kusahau alipokuwa ameiweka barakoa.

Kwenye video ambayo sasa imesambaa mtandaoni, Rais anaonekana akimaliza kuhutubia taifa na kisha kusahau alipokuwa ameweka barakoa yake.

Anatupa macho hapa na pale na kisha kuwageukia waliokuwepo na kuwapa macho ya simba mwenye hasira.

"Nani amechukua barakoa yangu jameni?" Rais anaskika akiguruma na ni wazi kutoka kwa video hiyo waliokuwepo wamebabaika.

Bila kusema chochote, wote wanatuoa macho hapa na pale na kisha kumuonyesha Rais alipokuwa ameiweka barakoa yake.

Licha ya kuwa tukio la angalau kuwavunja mbavu waliokuwepo, ni dhahiri katika nyuso zao kuwa hakukuwa na lolote la kutabasamu.

Rais anapoipata anavaa na kuanza kuondoka jukwaani bila mahanjam ambayo hushuhudiwa kwa kawaida katika yake na wanaomzunguka wakati wa vikao vya wanahabari.

Ni video ambayo ilizua kicheko mtandaoni wengi wakihisi Rais alikuwa kweli amechanganyikiwa.

Wengine wlishangaa iwapo inawezekana kwa mtu yeyote kuchukua maski ya kiongozi wa taifa ambaye hulindwa pakubwa.

Kwenye hotuba yake kwa taifa Ijumaa Machi 26, Rais Uhuru Kenyatta amefunga kaunti za Nairobi, Nakuru, Kajiado, Machakos na Kiambu.

Aidha mikutano yote pia imepigwa marufuku katika kaunti hizo huku kafyu ikiongezwa ambapo itakuwa ikianza saa mbili usiku hadi saa kumi asubuhi.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke