Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namibia yazuia meli inayoshukiwa kubeba shehena ya jeshi la Israel

Namibia Yazuia Meli Inayoshukiwa Kubeba Shehena Ya Jeshi La Israel.png Namibia yazuia meli inayoshukiwa kubeba shehena ya jeshi la Israel

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meli inayoshukiwa na mamlaka ya Namibia kubeba shehena ya kijeshi iliyokusudiwa kutumiwa katika vita vinavyoendelea Gaza imezuiwa kutia nanga katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Waziri wa Sheria wa Namibia Yvonne Dausab aliviambia vyombo vya habari vya serikali kuwa meli hiyo ilisimamishwa kwa sababu ilikuwa na "vifaa vyenye vilipuzi vinavyopelekwa Israel".

Meli ya MV Kathrin, ambayo ilianza safari kutoka Vietnam, ilikuwa imeomba ruhusa ya kutia nanga katika bandari ya Walvis Bay - kabla ya kuelekea kaskazini, kwenye njia inayoshukiwa kuelekea Mediterania kupitia Mlango Bahari wa Gibraltar.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalikuwa yameonya kwamba Namibia ingeweza kuhusishwa na ukiukaji wa haki za binadamu kama ingeruhusu meli hiyo kutia nanga.

Haijulikani ni kwa nini meli hiyo ilitaka kutia nanga, lakini vyombo vinavyosafiri kwa muda mrefu huwa vinasimama ili kupata mahitaji wanayohitaji kwa kipindi hicho, kupumzika, kupakua au kubeba mizigo.

Desemba mwaka jana, jirani na mshirika wa Namibia, Afrika Kusini walifungua kesi inayoendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ikidai Israel inafanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Israel imekanusha madai ya mauaji ya halaiki na kusema kuwa "hayana msingi".

Mzozo huo ulianza baada ya Hamas kuanzisha shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa kwa Israel tarehe 7 Oktoba, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 251 kuchukuliwa mateka.

Jeshi la Israel kisha lilianzisha kampeni ya kumaliza kundi la Hamas na zaidi ya watu 40,430 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live