Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namibia yakasirishwa na watalii waliopiga picha za utupu

Namibia Yakasirishwa Na Watalii Waliopiga Picha Za Utupu Namibia yakasirishwa na watalii waliopiga picha za utupu

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Namibia zimeshutumu watalii waliopiga picha uchi katika moja ya vivutio vya juu nchini humo - eneo la ‘Big Daddy dune’ katika jangwa la Namibia.

Baadhi ya wageni waliliambia gazeti moja la eneo hilo kuwa walishangazwa na tabia hiyo na kutaka watalii hao kuchukuliwa hatua.

Watalii hao ambao hawakutajwa majina wanaweza kuwekwa kwenye orodha ya wanaofungiwa kuingia katika hifadhi zozote za Namibia, msemaji wa wizara ya utalii aliviambia vyombo vya habari vya ndani.

Picha na video za watalii hao zilisambazwa kuzua hisia kali.

Kenneth Nependa, makamu mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Utalii vya Namibia, aliiambia tovuti ya habari ya Namibian Sun kwamba tabia hiyo inahatarisha kuvutia watalii "Inachukiza sana na kwa kweli [inaleta] taswira mbaya kwa Namibia,"

Bw Nependa alisema, akiongeza kuwa eneo la milima wa Big Daddy sio tu mahali pa kupumzika kwa watalii bali kwa familia pia.

Haijabainika ni nani alichukua picha hizo na video ya watalii hao watatu wa kiume, wanaoonekana wakiwa uchi kabisa kwenye kichanga, karibu na nguo zao.

Mamlaka haikujibu mara moja maswali ya BBC kuhusu utambulisho wa watalii hao.

Chanzo: Bbc