Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namibia yajipanga kukomesha umasikini

Namibiaa Namibiaa Namibia yajipanga kukomesha umasikini

Thu, 22 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Namibia imekusudia kufanyia marekebisho sheria yake ya sekta ya chakula ikijumuisha pia nyama maziwa na jamii ya ndege wa kufuga, ili kuimarisha uzalishaji wa chakula nchini humo na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje.

Hayo yamesemwa bungeni na Waziri wa Kilimo, Maji na Marekebisho ya Ardhi wa Namibia, Calle Schlettwein ambaye ameongeza kuwa, serikali ya nchi hiyo inalenga kuimarisha ushindani wa viwanda na kuboresha uwiano wa biashara nchini humo, kupitia kuingiza maziwa na bidhaa za jamii ya ndege wa kufuga hasa kuku ndani ya mfumo wa udhibiti.

Amesema, marekebisho hayo yatasaidia kudhibiti uingizaji wa kiholela wa bidhaa za maziwa na kuku na kuwasaidia wazalishaji wa ndani. Sekta ya ufugaji wa jamii ya ndege itaingizwa kwenye sheria mpya ya udhibiti nchini Namibia

Marekebisho yaliyowekwa katika mswada mpya ni pamoja na mabadiliko kadhaa muhimu. Kutatolewa ufafanuzi mpya maana ya mifugo na mazao na kuhusisha mpaka jamii ya kuku pamoja na wanyama au bidhaa nyingine yoyote ya nyama ambayo wizara itaona ni muhimu.

Zaidi ya hayo, Bodi ya Nyama ya Namibia ambayo inadhibiti tasnia ya nyama itabadilishwa jina na kuitwa Bodi ya Mifugo na Bidhaa za Mifugo ya Namibia ili kuendana na upana wa majukumu yake.

Serikali imewasilisha muswada bungeni ili kuwezesha usimamizi madhubuti. Muswada huo unapendekeza kuanzishwa mfumo mpya wa malipo ya ushuru kwa wazalishaji ambao utadhibitiwa sheria maalumu. Vile vile waziri husika atapewa mamlaka ya kutunga sheria ndogo kufanikisha jambo hilo.

Kwa mujibu wa Shirika la Usimamiaji wa Changamoto za Uchumi ambacho ni chombo cha kuangalia data za biashara ya kimataifa, Namibia inategemea bidhaa kutoka nje kwa asilimia 80 kwa ajli ya matumizi yake ya chakula na sehemu kubwa ya bidhaa hizo zinaingizwa nchini humo kutokea Afŕika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live