Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Namibia inakaribia kuwa na rais mwanamke wa Kwanza

Namibia Namibia inakaribia kuwa na rais mwanamke wa Kwanza

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: Voa

Chama kinachotawala nchini Namibia kimemteua Netumbo Nandi-Ndaitwah kama makam rais wake na hivyo kumueka katika nafasi nzuri ya kuwa mgombea wa urais wa kwanza mwanamke nchini humo, katika uchaguzi wa mwaka 2024 wakati rais wa nchi hiyo atakapostaafu.

Netumbo Nandi Ndaitwah ni naibu waziri mkuu katika serikali ya sasa, na uteuzi wake katika nafasi ya juu ya chama cha Swapo, umefanyika wakati wa kongamano kuu la chama.

Kulingana na katiba ya chama cha SWAPO, Nandi Ndaitwah atakuwa mgombea wake wa urais wakati rais wa sasa Hage Geingob atakapomaliza mihula yake miwili madarakani, ambayo imesalia miezi 15.

Ndaitwah amewashinda wagombea wengine wawili akiwemo waziri mkuu wa sasa katika uchaguzi uliohusisha wanachama wa ngazi ya juu 700 na kuhudhuriwa pia na viongozi wa chama kinachotawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF.

Chanzo: Voa