Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nairobi 'imezidiwa' na mafuriko - seneta

Mafuriko WhatsApp Nairobi 'imezidiwa' na mafuriko - seneta

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mafuriko katika mji mkuu wa Kenya Nairobi "yameongezeka hadi viwango vya juu" na mamlaka za mitaa "zimezidiwa," Seneta wa Nairibi ameonya.

Edwin Sifuna, ambaye anasimamia kaunti ya Nairobi, alizua taharuki kwenye mtandao wa kijamii wa X huku akichapisha picha zinazoonyesha mtaa mzima uliosombwa na mafuriko.

Katika klipu hiyo, wakazi wanaonekana wakiwa wamenaswa kwenye paa la nyumba yao.

Mamia ya wengine jijini Nairobi na maeneo ya karibu pia walikumbwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha.

"Tunahitaji huduma zote za dharura za kitaifa kuhamasishwa ili kuokoa maisha," Bw Sifuna alisema.

Taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa likishuhudia mvua kubwa kwa wiki kadhaa.

Jumatano asubuhi, Shirika la Reli la Kenya lilisema mafuriko hayo yameathiri njia za reli, na hivyo kufanya kuwa vigumu kwa treni kufanya kazi.

Kampuni hiyo ilisema hofu ya usalama iliilazimisha kusitisha huduma zake.

Barabara kuu, zikiwemo ile ya Mombasa na Thika, zilisombwa na maji ya mafuriko, na kusababisha msongamano wa magari nyakati za asubuhi

Barabara yenye shughuli nyingi ya Namanga, inayoelekea mpaka wa Tanzania, ilifurika baada ya Mto Athi ulio karibu kuvunja kingo zake Jumatano asubuhi.

Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya linasema timu zake za kukabiliana na mafuriko zinafanya kazi katika maeneo mengi yaliyoathiriwa na mafuriko, zikihamisha familia kwenye usalama na kutoa afua zingine za kuokoa maisha.

Wakazi wa baadhi ya mashamba jijini Nairobi pia wameachwa bila makao baada ya nyumba zao kuzama kutokana na mafuriko. Inatabiriwa kuendelea kunyesha.

Karibu watu 35 wamekufa tangu mwezi uliopita kutokana na mafuriko na zaidi ya 100,000 wameathirika, kulingana na Umoja wa Mataifa, ambao unaashiria takwimu za Shirika la Msalaba Mwekundu katika taarifa za hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live