Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amekosolewa na kuashiria nchi hiyo kama kampuni yenye hisa ambayo kwanza itawanufaisha waliopigia kura serikali.
Bw Gachagua alitetea uteuzi wa hivi majuzi wa serikali akisema waliomuunga mkono na Rais William Ruto walistahili "kuvuna kwanza".
“Serikali hii ni kama kampuni iliyodhaminiwa na hisa. Wapo wamiliki wa kampuni, wapo wenye hisa nyingi, wenye hisa chache na wasio na hisa. " Kama uliwekeza serikalini na sasa ni wakati wako wa kuvuna," alisema.
“Wapo wanaonilaumu kwa kusema hivi lakini ni makosa? Hata wale wakosoaji na wale ambao hawakutuunga mkono watavuna, lakini watalazimika kusubiri kilichobaki ili watu wajue wanapopiga kura, inamaanisha kitu na ina matokeo.
Kauli hiyo ilizua gumzo kali miongoni wa Wakenya katika mitandao kijamii huku wanaopinga wakisema serikali inafaa kuwahudumia Wakenya wote bila kujali misimamo yao ya kisias.
Wengine waliongeza kuwa wananchi wote wanastahili uangalizi sawa kutoka kwa serikali, ikiwa ni pamoja na linapokuja suala la miradi ya maendeleo.