Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu mkuu wa utawala kijeshi wa Sudan ayaita mapinduzi ya 2021 kuwa 'makosa'

Naibu Mkuu Wa Utawala Kijeshi Wa Sudan Ayaita Mapinduzi Ya 2021 Kuwa 'makosa' Naibu mkuu wa utawala kijeshi wa Sudan ayaita mapinduzi ya 2021 kuwa 'makosa'

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Naibu mkuu wa baraza tawala la Sudan, Mohamed Daglo, amesema mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2021 yalikuwa "makosa".

Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Bw Daglo alisema imetoa mwanya kwa utawala wa zamani wa Omar al-Bashir, ambaye aliondolewa madarakani miaka miwili kabla.

Alisema alikosea kutoa msaada katika mapinduzi ya hivi karibuni ni mojawapo ya makosa hayo.

Mpango wa Disemba wa kuibadilisha Sudan kuwa na utawala wa kiraia, Bw Daglo aliahidi kutekeleza mageuzi ya usalama, ikiwa ni pamoja na kuunganisha kundi lake la kijeshi la RSF katika jeshi la taifa.

Sudan imekuwa katika msukosuko wa kiuchumi na kisiasa tangu mwaka 2021, wakati Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alipopinduliwa na kuchukua madaraka kutoka kwa serikali ya mpito inayoongozwa kiraia na hivyo kuharibu mpito kwa utawala wa kiraia kufuatia kuondolewa kwa Bashir 2019.

Wanaharakati wanaounga mkono demokrasia wamekuwa wakiandaa maandamano dhidi ya mamlaka ya kijeshi tangu wakati huo.

Chanzo: Bbc