Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu gavana wa Siaya William Oduol arejea afisini chini ya ulinzi mkali

Naibu Gavana Wa Siaya William Oduol Arejea Afisini Chini Ya Ulinzi Mkali Naibu gavana wa Siaya William Oduol arejea afisini chini ya ulinzi mkali

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: Radio Jambo

Naibu Gavana wa Siaya anayekabiliwa na utata William Oduol alirejea afisini mwake siku ya Alhamisi na kupokelewa kwa njia tofauti na wafanyikazi wa kaunti na wakaazi wa eneo hilo.

Kuingia kwa ghafla kwa Oduol katika makao makuu ya kaunti hiyo kulishuhudia maafisa wa usalama wakiingia kwa haraka katika makao makuu ya serikali ya kaunti, huku umati wa watu ambao ulipata hisia za uwepo wake ukiongezeka haraka.

Milango ya jengo hilo ilifungiwa nje haraka na umma na vyombo vya habari kuamriwa kutoka nje na maafisa wa usalama.

Baada ya kukaa kwa takriban saa mbili ofisini mwake, Oduol, ambaye amejipata kwenye njia panda na gavana wake James Orengo aliondoka kutoka makao hayo chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi waliojihami na kuanza ziara katika mji wa Siaya, huku wananchi wakifuata.

Akihutubia umma katika soko la manispaa ya Siaya, Oduol alimtaka Orengo kuweka kando tofauti zao na kuongeza kuwa yeye na gavana wanapaswa kuungana kuhakikisha kuwa wakazi wa Siaya wanapata huduma bora.

"Wangu ni wito wa amani na upatanisho na ninataka kuhimiza uongozi wetu, viongozi wa kanisa na wazee wa Siaya kutuleta pamoja ili tuweze kubadilisha kaunti hii nzuri," Alisema Oduol.

Alisema anapanga hafla ya shukrani ambapo watu wa tabaka mbalimbali wataalikwa kujumuika naye kumshukuru Mungu kwa kumuepusha na mashitaka.

Naibu Gavana wa Siaya hivi majuzi alitimuliwa na bunge la kaunti uamuzi uliyobatilishwa na seneti.

Chanzo: Radio Jambo