Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Rais Ruto azikana mali alizotajiwa kuzimiliki

Fad95d2f73a96e5b Naibu Rais Ruto azikana mali alizotajiwa kuzimiliki

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto amekanusha kumiliki mali iliyowekwa wazi na Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i.

Amekanusha kumiliki mali iliyowekwa wazi na Matiang'i akisema hajui baadhi ya biashara zilizotajwaMatiang'i alisema kwa jumla DP Ruto ana ulinzi wa maafisa 257 na ni mmoja wa wanaolindwa sana nchini.

Ruto amesema Matiang'i alienda bungeni kutoa porojo ili kumpiga kisiasa DP badala ya kujadili kuhusu ulinzi wa DP.

Kupitia kwa msemaji wake David Mugonyi, Ruto amesema Matiang'i alienda bungeni kutoa porojo ili kumpiga kisiasa DP.

"Mali nyingi iliyodaiwa kumilikiwa na Naibu Rais kupitia taarifa bungeni si kweli, hiyo si mali yake. La kuchoma zaidi ni madai ya Mataing'i kuwa ametoa ulinzi kwa mali hii ambayo hatuijui," Mugonyi alisema.

Alisema Matiang'i ameamua kucheza siasa na mamlaka anayoshikilia badala ya kuhakikisha kuwa naibu rais ana usalama.

"Matiang'i amekuwa akitumia mamlaka yake vibaya kucheza siasa za kuhakikisha kuwa anamdhalilisha naibu rais kwa sababu za siasa," alisema Mugonyi



Taarifa ya Mugonyi ilisema Matiang'i ni waziri anayehisi kwamba DP Ruto haifai kupokea huduma za usalama.

Alikosoa hatua ya Matiang'i kulinganisha usalama wa DP na waliowahi kuhudumu kama makamu wa rais.

Alisema DP ana maafisa 257 kwa jumla na hivyo kuwa mmoja wa watu wanaolindwa pakubwa nchini.

Mugonyi alisema hatua ya Matiang'i kuanika baadhi ya mali ya Ruto ni njama nyingine ya kuweka usalama wake hatarini.

Kwa mujibu wa Matiang'i, Ruto ni mmiliki wa Kitengela Gas, hoteli ya Wetson pamoja na nyingine ukanda wa Pwani.

Ana shamba la kuku pia pamoja na boma kadhaa jijini Nairobi, Sugoi na Elgon View mjini Eldoret.

Ufichuzi wa waziri huyo ulizua hisia mseto mtandaoni huku wakosoaji wa DP wakitumia yaliyowekwa wazi kumlima.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke