Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Rais Ruto anunua trei moja ya mayai kwa Tsh. 207,470

838d0f418aeefc95 Naibu Rais Ruto anunua trei moja ya mayai kwa Tsh. 207,470

Fri, 22 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Naibu Rais William Ruto yuko katika ziara ya siku mbili kaunti ya Kakamega ambapo anafanya kampeni za uchaguzi mkuu wa 2022. Akiwa eneo hilo Ruto alinunua trei moja ya mayai kwa KSh 10,000 ambayo ni zaidi ya Tsh. Laki Mbili za Tanzania baada ya kuwahutubia wakazi wa Butere.

Awali akiwa ziarani Nyandarua, Ruto alimzawadi mwanamke mmoja KSh 100k baada ya kumtumbuiza. Naibu Rais William Ruto yuko katika ziara ya siku mbili kaunti ya Kakamega ambapo amekuwa akijipigia upatu huku uchaguzi wa 2022 ukikaribia.

Akiwahutubia wakazi wa eneo bunge la Butere ambapo lilikuwa mojawapo wa maeneo ambayo alizuru, Ruto alinunua trei ya mayai kwa KSh 10,000.

" Hebu na yule anayeuza mayai aje hapa, nataka kununua, mwajua mimi hufanya biashara ya mayai, mmesoma gazeti kweli? chukua hizi KSh 10k," Ruto alisema huku akishangiliwa na umati.

Mapema mwezi huu, Ruto alimzawadi mwanamke mmoja KSh 100,000 baada ya kumsaidia kuchuuza biashara yake eneo la Nyandarua kaunti ya Laikipia.

Mwanamke huyo aliyetambulika kama Mumbi alimtumbuiza Ruto akiimba nyimbo za kumlimbikizia sifa.

Akionekana kufurahishwa na Mumbi, Ruto alimuita jukwani na kumkabidhi KSh 100, 000.

"Si huyu ameweza:, hebu na tumpigie makofi, Mumbi, nataka kukushukuru kwa wimbo huu na jinsi umenitumbuiza, hizi hapa KSh 100k uende kuendeleze biashara yako," Ruto alisema huku akimkabidhi pesa hizo.

Aidha, akizuru kaunti ya Migori mwezi jana, Ruto tena aliacha sifa baada ya kumpokeza mwanamke KSh 20k ambaye alikuwa amemuazima mwavuli wake wakati kulikuwa kukinyesha.

Ruto alikuwa anawahutubia wakazi wa mji wa Awendo wakati mvua ilianza kumyeshea.

Naibu Rais ametangaza kuwania kiti cha urais katika chaguzi mkuu ujao kupitia kwa tiketi ya chama cha UDA ambacho amekuwa akizunguka kote nchini akikipigia upato.

Ruto anatarajiwa kumenyana na wagombea kadhaa wa urais akiwemo Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ambaye pia mi mpinzani wake mkuu.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke