Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Rais Ruto amemjibu Rais Uhuru "Acha makasiriko, siondoki"

8295f46a38ca1b1e Naibu Rais Ruto amemjibu Rais Uhuru "Acha makasiriko, siondoki"

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

DP Ruto anaendelea kuwa kichwa ngumu kwa mdosi wake huku akipuuza wito wa kujiuzulu uliotolewa na UhuruDP alisema Rais yuko na makasiriko na anafaa kutulia kwani hawezi kujiuzulu kutoka serikaliniRais Uhuru Jumatatu alimtaka DP kujiuzulu kutoka serikali yake akisema anaichoma mwiba akiwa ndaniNipe nikupe kati ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto zinaonekana kuendelea baada ya urafiki wao kisiasa kufifia.

Siku moja tu baada ya Rais Uhuru kumtaka kujiuzulu kutoka serikali yake akisema amekuwa akiichoma kutoka ndani, DP amemjibu.

Akiongea huko Taita Taveta Jumanne, Agosti 24 Ruto alimwambia Rais kuwa atangoja sana kwani yeye hana mpango wowote wa kuondoka serikalini.

"Kwa wale ambao wako na shida, nataka niwaombe msamaha na ninataka niwaambie niko na ajenda. Sina wakati wa kurudi nyuma wala kutii amri . . .

niko na ajenda ya kuhakikisha kuwa wasio na kazi, wanaoendesha biashara ndogo na wakulima wanaong'ang'ana wamehusishwa katika uongozi. Kenya si mali ya viongozi na kile wanachotaka," alisema Ruto



Alimwambia Rais kuwa yeye ameamua kuhakikisha mfumo wa kiuchumi umebadilishwa na hawezi kuacha kurindima siasa hizo.

"Siwezi kujiondoa kwa sasa tumeamua tutabadilisha uchumi na tutakuwa na mfumo ambao utawainua Wakenya wasio na kazi na kuwainua walio na biashara ndogo ili tujenge Kenya ambapo kila mmoja anahusishwa," aliongeza Ruto

Alitaja matamshi ya Rais kuhusu hulka zake za kuikosoa serikali kama makasiriko na kumtaka kutuliza boli.

“Kenya ni yetu wote… Hakuna haja ya vurugu hakuna haja ya makasiriko," alisema



Akiongea kwenye mahojiano na wanahariri katika Ikulu Jumatatu, Rais alisema hajui kiini chaa tofauti kati yake na DP Ruto.

Alisema tatizo kubwa la DP ni kupiga vita juhudi zake za kuwaleta pamoja viongozi na hivyo kuamua kumuwacha nje ya mipango yake.
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke