Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Rais Kenya aondolea Madarakani

Gy41rntxoaea0su E1727951695871 Naibu wa Rais nchini Kenya Rigathi Gachagua

Fri, 18 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu wa Rais nchini Kenya Rigathi Gachagua ameondolewa madarakani na bunge la Seneti nchini humo baada ya Maseneta kupiga kura kuhusu mashtaka 11 yaliyokuwa yakimkabili.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 145 kinachosomwa pamoja na Kifungu cha 150(1)(b) na (2) cha Katiba na amri ya kusimama ya 78 na 79 ya Kanuni za Kusimamia Seneti, Seneti imekubaliana kumwondoa madarakani, Mhe. Rigathi Gachagua, EGH, Naibu Rais wa Jamhuri ya Kenya, kwa MSINGI WA 2: Uvunjaji mkubwa wa vifungu vya 147(1) na 152(1) vya Katiba kwa kumdhoofisha Rais na Baraza la Mawaziri na kutatiza utekelezaji wa majukumu ya utawala wa serikali kuu.

Hesabu:

• Jumla ya kura: 42 • Kura 21 ziliunga mkono, sawa na asilimia 50.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live