Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Gavana wa Kericho Susan Kikwai Azikwa baada ya kuangamizwa na Covid-19

43b175b96ef6c8df Naibu Gavana wa Kericho Susan Kikwai Azikwa baada ya kuangamizwa na Covid-19

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Susan Kikwai ambaye alikuwa akihudumu kwa muhula wake wa pili kama naibu Gavana wa Kericho alifariki dunia Jumamosi, Machi 20

- Kikwai ambaye aliangamizwa na virusi vya COVID-19 alizikwa kufuatia masharti ya wizara ya afya ya kuzuia maambukizi zaidi ya virusi hivyo

- Kila mtu anayepoteza maisha yake kwa sasa kutokana na virusi hivyo anapaswa kuzikwa chini ya saa 72 kama vile serikali ilivyoamuru

- Kikwai alizikwa nyumbani kwa babake eneo la Kipkelion Jumanne, Machi 21 huku waombolezaji wachache wakihudhuria mazishi yake

Naibu Gavana wa kaunti ya Kericho Susan Kikwai ambaye aliangamizwa na virusi vya COVID-19 Jumamosi, Machi 20 amezikwa nyumbani kwa babake eneo bunge la Kipkelion

Kikwai alizikwa Jumanne, Machi 23 kulingana na masharti yaliowekwa na wizara ya afya kuhusu kuzuia msambao wa virusi vya Covid -19.

Mwili wake ulisafirishwa kutoka mochuari ya Siloam mjini Kericho hadi nyumbani kwao mwendo wa saa tatu asubuhi.

Wanasiasa wa bunge la kaunti ya Kericho walifanya maombi maalumu ya kumuaga kiongozi huyo Jumatatu, Machi 22.

" Tumefika hapa ili kuiombea familia ya mwendazake mama Susan Kikwai, najua kuna viongozi ambao hawataweza kufika mazishini na ndio sababu tumeamua kufanya maombi hapa bungeni,"Alisema spika wa bunge la Kericho.

" Wakenya wamelegeza sana kuzingatia masharti ya Covid -19 na ndio sababu maafa na maambukizi mengi yanazidi kuripotiwa nchini," Aliongezea spika huyo.

Kikwai mwenye umri wa miaka 60 amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu.

Marehemu Kikwai alikuwa akihudumu kwa muhula wake wa pili kama naibu Gavana wa kaunti hiyo, alichaguliwa mwaka wa 2013 na pia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke