Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nahodha Gor Mahia wachezaji saba aomba radhi mashabiki

0c9a64bc279d5249987810f9d673c0ed.png Nahodha Gor Mahia wachezaji saba aomba radhi mashabiki

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

NAHODHA Msaidizi wa Gor Mahia, Phillemon Otieno ameomba radhi mashabiki wao na wa soka Kenya kufuatia kufungwa mabao 6-0 na CR Belouizdad Algeria mwishoni mwa wiki iliyopita.

Gor ilipoteza mechi hiyo dhidi ya mabingwa hao wa Algeria ikiwa ni mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza na kuondoa matumaini ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa. Ili mabingwa hao wa Kenya wafuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo wanatakiwa kushinda mabao 7-0 katika mechi ya marudiano wiki ijayo.

Ikishindikana, mabingwa hao wa Algeria watakwenda hatua ya makundi na kuaiacha Gor ikiangukia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho. Otieno ambaye aliiongoza timu baada ya nahodha Kenneth Muguna kuwa majeruhi, licha ya fedheha hiyo alisema timu imepata somo.

“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu naomba radhi kwa mechi tuliyopoteza dhidi ya Belouizdad. Ni soka na tunajifunza kwa makosa, ni ishara tumepewa kupambana kama tunataka kufanikiwa malengo yetu msimu huu,” alisema.

Katika mechi hiyo, Gor walikuwa nyuma kwa mabao manne mpaka mapumziko kabla ya kufungwa mawili dakika za mwisho za kipindi cha pili. Wanatarajia kuwakaribisha wageni wao kwenye uwanja wa Nyayo Januari 6.

Chanzo: habarileo.co.tz