Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NPS: Video inayosambazwa mitandaoni ikimuonesha askari akipokonywa simu ni feki

A7756a11205e6877 NPS: Video inayosambazwa mitandaoni ikimuonesha askari akipokonywa simu ni feki

Fri, 9 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Afisa huyo wa polisi ambaye hajafahamika anadhaniwa kuwa mwathiriwa wa majambazi waporaji wa Nairobi baada ya mwizi aliyekuwa kwenye pikipiki kunyakua simu yake Walakini, Huduma ya Polisi imesisitiza kwamba video hiyo ni feki na ilitengenezwa ili kuchafua sifa nzuri ya jeshi lenye nidhamu Afisa huyo wa polisi alikuwa akiongoza magari barabarani kwenye mzunguko wa mtaani Roysambu Jumanne, Julai 6, wakati tukio hilo lilipotokeaHuduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) imepuuzilia mbali video inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii ikionyesha afisa wa polisi akiporwa simu na wanaodhaniwa kuwa wezi.

Kwenye video hiyo, afisa huyo wa polisi ambaye hajatajwa jina anasemekana kuwa mwathiriwa wa majambazi wa Nairobi baada ya mwizi aliyekuwa kwenye pikipiki kumpokonya simu.

Kupitia Twitter Jumatano, Julai 7, Hillary Mutyambai ambaye huiongoza huduma hiyo alisisitiza kwamba video hiyo ilitengenezwa ili kuchafua sifa nzuri ya jeshi lenye nidhamu.

"Uchunguzi wetu umebaini kuwa video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai kuonyesha afisa wa polisi anayenyang'anywa simu ni video yenye nia mbaya. Tunawasihi umma kuipuuza," ulisema ujumbe wa Tweeter kutoka kwa huduma hiyo.

Afisa huyo wa polisi alikuwa akiongoza magari barabarani kwenye mzunguko wa mtaani Roysambu Jumanne, Julai 6, wakati tukio hilo lilipotokea.

Video hiyo iliyonaswa na kamera ya garini ilionyesha kuwa tukio hilo lilitokea mwendo wa 5pm.

Katika video hiyo, bodaboda mbili zinaoneka huku ya kwanza ikimpita afisa huyo wa polisi aliyekuwa akizungumza kwa simu, na kufuatwa na ya pili ambayo abiria wake anampokonya simu afisa huyo na kutokomea.

Raia kupigana na polisi wa trafikiMnamo Desemba 24 2020, kulitokea sarakasi ya Krismasi wakati afisa wa polisi na dereva mmoja kuswagana mangumi.

Sinema lilianza pale afisa trafiki anayesimamia barabara kuu ya Nakuru-Nairobi kugonga gari la dereva huyo akitumia rungu yake wakati wa msongamano mkubwa wa trafiki.

Akiwa amekasirishwa na kitendo cha afisa huyo, dereva ambaye hakutajwa jina alitoka garini akitaka kujua ni kwanini afisa huyo alikuwa amegonga gari lake.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke