Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NGORONGORO, UGANDA KUPIMANA UBAVU

61d8e2f100b90a4906a7f9c953e33b80 NGORONGORO, UGANDA KUPIMANA UBAVU

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ itamenyana na Uganda katika mchezo wa kimataifa wa kirafi ki utakaochezwa leo saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kocha Mkuu wa Ngorongoro, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ aliliambia gazeti hili Dar es Salaam jana kuwa kikosi chake kimefanya maandalizi mazuri kuhakikisha kinautumia vyema mchezo huo kujiimarisha kabla ya kuelekea Mauritania katika michuano ya fainali za Afrika ‘Afcon’ kwa vijana wa umri huo.

“Kikosi chetu kinaendelea vizuri, wachezaji wako tayari kupambana na Uganda na tunajua ni timu ya aina gani, mara ya mwisho tulikutana katika michuano ya kufuzu wakatufunga kwa hiyo ni kipimo kizuri kwetu,” alisema.

Alisema ana amini mchezo huo utawapa taswira ya kule wanakoelekea katika michuano ya Afcon baadaye mwezi huu. Awali, michuano hiyo maalum pia ilikuwa ishirikishe Namibia lakini timu hiyo imeshindwa kuja nchini kutokana na changamoto ya virusi vya corona nchini kwao hivyo Tanzania itacheza mara mbili na Uganda.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana kwenye michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) mchezo wa fainali na Uganda kushinda mabao 4-1. Ngorongoro Heroes iliingia kambini kwa zaidi ya wiki mbili na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki ya kujipima nguvu dhidi ya timu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza.

Chanzo: habarileo.co.tz