Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo waibuka baada ya Saudi Arabia kuwarejesha nyumbani Wanigeria

Mzozo Waibuka Baada Ya Saudi Arabia Kuwarejesha Nyumbani Wanigeria Mzozo waibuka baada ya Saudi Arabia kuwarejesha nyumbani Wanigeria

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mzozo umeibuka kufuatia hatu aya Saudi Arabia kuwarejesha nyumbani Wanigeria 177 siku ya Jumatatu, muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Jeddah.

Mamlaka ya Saudia iliripotiwa kufutilia mbali visa ya Wanigeria hao walipokuwa safarini kwa sababu zisizojulikana, lakini wakawaondoa wengine 87 kwenye ndege ya Air Peace ya abiria 264.

Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Nigeria siku ya Jumatano ulisema kwamba abiria waliorejeshwa "hawakutimiza masharti ya kuingia" na "waliwasilisha taarifa zisizo sahihi ili kupata aina ya visa ambayo haiwahusu, ambayo iligunduliwa wakati wa kuwasili".

Lakini Air Peace imepinga kauli ya Saudi Arabia, ikisema Jumatano kwamba vhati ya usafiri ya abiria wote "zilihakikiwa kuwa halali" kwa kutumia mifumo ya uthibitishaji ya Saudi Arabia kabla ya kuingia.

Shirika hilo la ndege liliongeza kuwa lilituma ilani ya abiria kwa mamlaka ya Saudia kabla ya kuondoka lakini hawakufuta visa yoyote au kuibua wasiwasi wowote wakati huo.

Siku ya Jumanne, wizara ya mambo ya nje ya Nigeria ilisema kuwa Wanigeria 18 waliorejeshwa walizuiliwa kuingia kwa sababu na rekodi za uhalifu na walipigwa marufuku kutoka nchini humo.

Wengi wa Wanigeria waliorejeshwa waliripotiwa kusafiri kwa ajili ya kuhiji katika mji mtakatifu wa Mecca.

Chanzo: Bbc