Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa bwawa la mto Nile wazua cheche za maneno kati ya Ethiopia na Misri

Nile Cruise Egypt 63c7bab066af Mzozo wa bwawa la mto Nile wazua cheche za maneno kati ya Ethiopia na Misri

Fri, 10 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya kuvumiliana iliimarishwa, lakini matamshi ya wawakilishi wa Msri na wenzao wa Ethiopia yalifichua ugomvi ambao ulikuwa haufichiki.

Mkutano wa hivi karibuni wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuzungumzia bwawa kubwa la Umeme linalomilikiwa na Ethiopia , kwa jina Grand Reneisance Dam (Gerd) linalotoa maji kutoka kwa mto Nile ulifanyika kwa njia ya video.

Sharti la kutokaribiana ambalo liliheshimiwa na waliohudhuria lilisisitiza tofauti ya kidiplomasia iliokuwepo. Ni tofauti zinazotishia na kusababisha hali ya kutoaminiana kati ya raia wa mataifa hayo mawili.

Bwawa hilo lililopo katika mto Nile lipo karibu na Misri na lina uwezo wa kudhibiti maji yanayoingia nchini humo ambayo yanategemewa sana na taifa hilo la kaskazini mwa Afrika. Presentational white space

Ujenzi wake utakapokamilika , litakuwa bwawa kubwa la umeme barani Afrika , na kutabiriwa kutoa umeme kwa raia milioni 65 wa Ethiopia , ambao kwa sasa hawana chanzo cha kupata umeme mara kwa mara. Ujenzi huo ulioanza 2011 unakaribia kukamilika.

Kwa wawakilishi wa Ethiopia na Misri katika mkutano huo wa UN, uwepo wa mataifa yao upo hatarini.

Tishio la uwepo wa mataifa hayo mawili limezuka na linaweza kuingilia chanzo pekee cha maisha ya takriban Wamisri milioni 100, kulingana waziri wa masuala ya kigeni nchini humo Sameh Shoukry.

Akitumia lugha kama hiyo, balozi wa Ethiopia katika Umoja wa Mataifa Taye Atske-Selassie alijibu: Kwa Ethiopia kutumia maji yake sio suala la kuchagua ,bali ni la umuhimu mkubwa. Wakati wa kujaza bwawa hilo

Matamshi hayo huenda yakaficha kwamba baada ya karibia muongo mmoja wa mazungumzo , yamekubaliana mambo mengi , lakini suali muhimu kuhusu jinsi na lini kujaza bwawa hilo na kiwango gani cha maji kinachopaswa kutolewa ndio mambo ambayo hayajatatuliwa.

Kufuatia miaka kadhaa ya mazungumzo yaliohusisha wataalam , makubaliano ya kikanuni kati ya Misri, Ethiopia na Sudan ambalo ndio taifa la tatu lililoathirika hayajatatua masuala hayo.

Na sasa tupo katika kipindi ambapo Ethiopia inasema itaanza kulijaza bwawa hilo katika kipindi cha wiki chache zijazo wakati wa msimu wa mvua.

Ni mpango ambao unatarajiwa kuchukua miaka saba.

Kwa Ethiopia , hatua ya kulijenga na kulijaza maji bwawa hilo sio la wakati tofauti alisema mmoja ya wawakilishi wa taifa hilo Zerihun Abebe akizungumza na BBC.

''Wamisri walijaribu kuwachanganya maafisa wa jamii ya kimataifa kwa kusema kwamba ni mambo tofauti'', aliongezea na kuhoji kwamba tamko la kanuni la 2015 kati ya mataifa hayo mawili liliruhusu Ethiopia kuendelea na mpango wake.

Lakini hivi sivyo Misri inavyofikiria

Baada ya Marekani na benki ya dunia kuhusishwa mwisho wa mwaka jana lakini zikashindwa kuishawishi Ethiopia kutia saini hati iliokubaliwa na Misri mwezi Februari, Muungano wa Afrika AU sasa umesema kwamba utajaribu kutafuta suluhu.

Iwapo maneno ya waziri wa masuala ya kigeni nchini Misri yatatiliwa maanani basi makubaliano yanahitajika haraka iwezekanavyo. 'Mikataba ya enzi za kikoloni'

"Uendeshaji na kujazwa maji kwa bwawa hilo bila makubaliano yanayohusisha hatua za tahadhari dhidi ya jamii zinazoishi chini yake huenda ukasababisha hofu na kuzua mgogoro ambao huenda ukaathiri usalama wa eneo ambalo tayari hali yake ni tete.," alionya bwana Shoukry.

Kwa upande wake, Ethiopia ilisema kwamba inataka kufanya majadiliano chini ya Muungano wa Afrika, badala ya UN , lakini ikailaumu Misri kwa usisitizaji wake juu ya haki za kihistoria na utumiaji wa sasa".

Haki hizo kulingana na Misri zilianzia mwaka 1929, wakati serikali ya Uingereza ilipotambua haki asilia na zile za kihistoria za Misri kuhusu maji ya mto Nile.

Pia iliipatia Misri haki ya kufanya mradi wowote kati maji hayo.

Mwaka 1959, Misri na Sudan zilitia saini makubaliano ambapo mataifa hayo mawili yalikubaliana kugawana raslimali za mto Nile huku Msri ikichukua maji mengi.

Hakuna taifa jingine lililotajwa kati ya mataifa 9 ambayo maji hayo yanapitia ikiwemo Ethiopia ambalo ndio chanzo cha mto Blue Nile.

Maji hayo ambayo yanaungana na maji ya mto mweupe ama White Nile katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, hutoa karibu 80% ya mtiririko mzima wa maji ya mto huo na Ethiopia inaona sio haki kwamba haiwezi kutumia fursa ya raslimali hiyo , Bwana Zerihun alisema.

''Iwapo Ethiopia itakubali kuachilia kiwango fulani cha maji kuelekea Misri kila mwaka basi hatua hiyo itathibitisha fursa ya kikoloni inayofurahiwa na taifa kama Misri. Ni kama ukoloni mambo leo na hilo halitakubalika'', aliongezea.

Ukweli ni kwamba Ethiopia inailaumu Misri kwa kutaka kuendeleza mtiririko huo wa maji ambao fursa ya utumizi wake walipatiwa 1959.

Ethiopia inasema kwamba wakati itakapokuwa ikilijaza maji bwawa hilo kwa mwaka wa pili, itaachiliwa maji yenye ujazo wa mita bilioni 31 kupitia bwawa hilo, lakini zaidi ya hilo haiwezi kulazimishwa kutoa kiwango fulani.

Usisitizaji wa kuwachilia kiwango fulani cha maji kwenda Misri licha ya kujali iwapo mvua itanyesha au la unaweza kumaanisha kwamba bwawa hilo halitaweza kufanya kazi wakati wa kiangazi.

Misri ina wasiwasi kuhusu kiwango cha maji ambacho itakuwa ikipokea.

Mataifa yalioungana chini ya bwawa hilo.

uwepo wa joto jingi baada ya miaka tisa ya mazungumzo huenda ukaonesha ukweli kwamba huu ndio mwisho wa kidiplomasia badala ya makubaliano na mambo huenda yakapoa hivi karibuni.

Lakini viongozi wote wawili wa Misri Abdula fattah al Sisi na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed pia wana mahitaji ya kisiasa katika mataifa yao na raia ambao wamejikita katika siasa za suala hilo.

Nchini Ethiopia, raia wamewekeza katika bwawa hilo. Gharama ya dola bilioni 4 ya mradi huo imeafikiwa kupitia kuwashawishi raia wa taifa hilo nyumbani na ughaibuni kuikopesha serikali fedha kupitia ununuzi wa dhamana.

Huku Abiy akikabiliwa na changamoto za kisiasa ambazo zimeathiri umaarufu wake , bwawa la Gerd ni suala ambalo raia wako tayari kumuunga mkono.

Baadhi ya raia hao wamechapisha kanda za video katika mtandao wa TikTok ili kuelezea suala hilo kwa kutumia vikombe na majagi ya maj

Kanda moja ambayo imetazamwa sana inamuonesha mwanamke akiwa na jagi , akiiwakilisha Ethiopia , akimwaga maji katika vikombe viwili vidogo na kusema kwamba taifa lake lina udhibiti.

Misri nayo imetengeneza kanda zake za video, huku moja ikidai kwamba bwawa hilo huenda likashambuliwa.

Kwa jumla, vyombo vya habari vya Misri vimekuwa vikiunga mkono serikali katika mazungumzo ya bwawa hilo , huku baadhi yao vikilaumu Ethiopia kwa kutotaka kushirikiana wakati wa mzozo huo.

Huku Vyombo vya habari katika mataifa hayo mawili vikitaka kupandisha joto la mzozo huo, ni kazi ya wanadiplomasia kujaribu kupoza hali ilivyo.

Bado haijulikani , iwapo wale wanaohusishwa katika mazungumzo hayo wanachukua jukumu hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live