Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa ajira Jumuiya ya Afrika Mashariki utata mtupu

Beeac Mzozo ajira za EAC wachukua sura mpya

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mzozo wa ugawaji ajira katika ofisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliodumu kwa tarkribani miaka 10 umejadiliwa tena na bunge la Jumuiya hiyo mapema Oktoba 15,2021 na kufikia muafaka wa kutoajiri makarani wa bunge hilo kwani kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za kuajiri.

Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya wabunge hao kutoridhishwa na viwango vya elimu vya makarani na manaibu wa bunge hilo kutumika katika nafasi za juu ndani ya jumuiya hiyo.

Inaelezwa kuwa wabunge kutoka Uganda wakiongozwa na Denis Namara, wamekuwa mstari wa mbele katika harakati za kutafuta usawa kwenye zoezi zima la kuajiri wafanyakazi hao.

Vikao vya bunge hilo vilianza Oktoba 3,2021 na vinatarajiwa kumalizika Oktoba 20,2021.

Hata hivyo mapema mwanzo wa mwaka 2021 zilitangazwa nafasi 60 za kazi kwenye Jumuiya hiyo jambo ambalo imeibua vuta ni kuvute kwa nchi wanachama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live