Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe Ethiopia

Ethiopia445 Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe Ethiopia

Fri, 10 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mzozo katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia umegeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vinatishia kusambaratisha nchi hiyo na kuyumbisha eneo lote.

Waasi wameanzisha mashambulizi eneo la kusini kuelekea mji mkuu wa shirikisho, Addis Ababa, na kumfanya Waziri Mkuu Abiy Ahmed - mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel na kanali wa zamani wa Luteni - kuliongoza jeshi la taifa kwenda vitani.

Ongezeko hilo la ghasia limesababisha raia wa mataifa ya magharibi na wafanyakazi wa kigeni wasio wa lazima wa Umoja wa Mataifa (UN) kuondoka nchini, bbaada ya usalama kuwa mbaya.

Baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1970 na 1980, Ethiopia ilikuwa moja ya nchi zinazokua kwa kasi kiuchumi barani Afrika na nguzo ya utulivu wa kikanda.

Lakini ghasia zimesambaa kutoka ngome ya waasi ya Tigray ambako mapigano yalizuka, hadi maeneo jirani ya Amhara kaskazini -magharibi na Afarkaskazini -mashariki.

Ushindi wa hivi majuzi wa vikosi vya muungano katika uwanja wa vita haujafanya chochote kuzima hofu ya kuongezeka kwa mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya mamia ya watu na maelfu ya wengine kuyahama makazi yao.

TPLF 'kurejea mara ya pili'

Waasi wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) wanasema uvamizi wao kuelekea kusini unalenga kushinikiza serikali kuondoa vikosi vyake eneo Tigray ambako mawasiliano na misaada ya kibinadamu imedhibitiwa.

Hata hivyo, utawala wa Abiy umewashtumu waasi kwa kueneza vurugu na kutaka mabadiliko ya utawal kwa nguvu, na hivyo kuzua hofu kwamba TPLF ina nia ya kurejea madarakani.

Chama cha TPLF kilitawala ngome ya kisiasa ya Ethiopia kwa miaka 27 baada ya kuanzisha uasi kama huo mwaka 1991 dhidi ya serikali ya wakati huo ya kikomunisti.

Utawala wao ulisababisha uwekezaji mkubwa katika miundombinu, ambayo ilikuza uchumi wa Ethiopia, lakini ilikumbwa na ukandamizaji wa kijamii na kisiasa.

Hali ambayo ilitibua maandamano makubwa dhidi ya serikali na kumweka madarakani Bw. Abiy mnamo Aprili 2018, ambapo alianzisha mageuzi ya kijamii, kisiasa na kiusalama.

Katika mapambano yake dhidi ya serikali, TPLF imeunda miungano ili kuongeza nguvu zake za mapigano na kuongeza sifa zake baada ya kuungwa mkono na vyama kadhaa vyenye mfungamano wa kikabila vinavyompinga waziri mkuu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live