Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Sudan waathiri uchumi wa nchi jirani

Mzozo Wa Sudan Waathiri Uchumi Wa Nchi Jirani Mzozo wa Sudan waathiri uchumi wa nchi jirani

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: Bbc

Mgogoro unaoendelea nchini Sudan umezua mzozo wa kikanda ambao una athari za kiusalama na kiuchumi, afisa mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) mjini Geneva, ameonya.

"Athari za mgogoro huu kwa Sudan Kusini ni nyingi - kuna athari za kiuchumi ambazo ni mbaya sana kwa sababu maeneo mazuri ya sehemu ya kaskazini ya Sudan Kusini yanategemea sana uchumi wa Sudan," alisema Kamishna Mkuu Msaidizi wa Operesheni wa UNHCR. Raouf Mazou.

"Kwa hivyo, ni mzozo wa kikanda unaozingatia masuala ya kiusalama, lakini pia mazingatio muhimu sana ya kiuchumi," Bw Mazou aliendelea, akiongeza kuwa Chad pia imeelezea wasiwasi kama huo.

Tangu kuanza kwa mzozo nchini Sudan mwezi Aprili, wakimbizi wamekimbia kuvuka mpaka na kuelekea Sudan Kusini, wengi wao wakiwa ni raia wa Sudan Kusini waliorejea nchini humo ambao sasa wanarejea nchini walikokuwa wamelazimika kukimbia.

Wanawasili pamoja na wakimbizi kutoka Sudan na nchi nyingine mbalimbali. Idadi ya wakimbizi wapya waliowasili Sudan Kusini wiki hii imepita100,000, UNHCR inasema. Bw Mazou aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu, Juba, Jumanne kwamba takriban wakimbizi 7,000 waliosajiliwa wameingia Sudan Kusini tangu mzozo nchini Sudan uanze.

Miongoni mwao walikuwa wakimbizi 3,500 wa Sudan, Waethiopia 2,600, Waeritrea 1,800 na mataifa mengine. Bw Mazou alisema kwa jumla, wakimbizi 400,000 wa Sudan wameikimbia Sudan na kuelekea nchi jirani. Soma zaidi: Wakimbizi wa Eritrea walinaswa kati ya migogoro miwili.

Chanzo: Bbc