Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Sudan: RSF yachukua udhibiti wa mji wa Nyala huko Darfur

Mzozo Wa Sudan: RSF Yachukua Udhibiti Wa Mji Wa Nyala Huko Darfur Mzozo wa Sudan: RSF yachukua udhibiti wa mji wa Nyala huko Darfur

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Kikosi cha kijeshi cha Rapid Support Forces (RSF) kimetwaa udhibiti wa mji wa pili kwa ukubwa nchini Sudan, Nyala, kutoka kwa jeshi baada ya mapigano ya miezi kadhaa, duru kadhaa zimeiambia BBC.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo alisema wakazi walikuwa wakisherehekea kwa sababu walitumai ingemaanisha kukomesha ghasia hizo.

Mapigano hayo yamewalazimu zaidi ya watu 670,000 kukimbia makazi yao.

Hospitali za jiji hilo zimeharibiwa, na maiti zinasemekana kuzagaa barabarani.

Hatua hii kubwa ya RSF inakuja wakati pande hizo mbili zinazozozana zikipangwa kuanza tena mazungumzo ya amani nchini Saudi Arabia.

Jeshi halijazungumzia kushindwa kwake huko Nyala. Nyala, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini, ni mji wa kimkakati unaounganisha Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

RSF ilianzia Darfur na imekuwa ikishutumiwa kwa ukatili dhidi ya makundi yasiyo ya Kiarabu katika eneo hilo wakati wa mzozo wa mwaka huu.

Majenerali wa ngazi za juu wa jeshi akiwemo mkuu wa jeshi huko Nyala waliuawa katika vita wiki chache zilizopita.

Kamanda wa pili wa RSF Abdulrahim Daglo, ambaye aliidhinishwa na Marekani kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya kikabila huko Darfur Magharibi, aliongoza kutekwa kwa Nyala.

Walioshuhudia wameripoti kuwa wapiganaji wa RSF wamekuwa wakipora na kuvamia nyumba za raia tangu walipouteka mji huo. Shirika la matibabu la Emergency linalotoa matibabu kwa waathiriwa wa vita, linasema wafanyakazi wake wa Sudan walichukuliwa kutoka kituo cha watoto huko Nyala na kukamatwa na RSF.

Mnamo Juni RSF iliteka Um-Dafog, mji mdogo kwenye mpaka na CAR ambao unaaminika kuwa eneo muhimu kwa mnyororo wao wa usambazaji.

Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umeshutumiwa kwa kusambaza silaha kwa RSF kupitia CAR na Um-Dafog wa Chad. UAE Imekanusha tuhuma hizo.

Chanzo: Bbc