Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Sudan: RSF yachukua udhibiti wa mji wa Darfur Kusini

RSF Mzozo wa Sudan: RSF yachukua udhibiti wa mji wa Darfur Kusini

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Kikosi cha wanamgambo kinachopigana dhidi ya jeshi nchini Sudan kimechukua udhibiti wa mji wa Darfur Kusini huku kukiwa na ripoti zaidi za ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mapigano kati ya Wanajeshi wa Rapid Support Forces (RSF) na jeshi yamesababisha maelfu ya familia kuukimbia mji wa Kas.

Kuna ripoti za wapiganaji wa RSF kupora au kuharibu majengo na masoko ya serikali.

Tangu vita vilipozuka katikati ya mwezi wa Aprili jumuiya zisizo za Kiarabu kote Darfur zimekuwa zikilengwa na RSF na wanamgambo washirika wa Kiarabu.

Mapigano makali yanaendelea katika mji mkuu, Khartoum, na katika maeneo mengine kadhaa huku juhudi za upatanishi za kikanda na kimataifa zikiendelea kumaliza mzozo huo.

Visa sawia vya ghasia za kikabila vilifanyika miongo miwili iliyopita wakati wanamgambo walipotumwa kukomesha uasi.

Vita hivyo vilisababisha vifo vya takriban watu 300,000.

Chanzo: Bbc