Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Sudan: Maji na umeme havipo huku mapigano yakiendelea

Mzozo Wa Sudan: Maji Na Umeme Havipo Huku Mapigano Yakiendelea Mzozo wa Sudan: Maji na umeme havipo huku mapigano yakiendelea

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mkazi mmoja katika mji mkuu wa Sudan ameiambia BBC kwamba hana tena maji ya kunywa huku mapigano kati ya vikosi pinzani yakiendelea mjini Khartoum kwa siku ya nne.

"Leo asubuhi tumeishiwa," Duaa Tariq alisema, akiongeza kuwa alikuwa akihifadhi chupa moja kwa ajili ya mtoto wake wa miaka miwili pekee.

Juhudi za kulirai jeshi na kundi la wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) kukubaliana kusitisha mapigano zinalegalega.

RSF imekuwa ikipora nyumba katika baadhi ya maeneo ya makazi ya mji mkuu.

Milipuko mikubwa ya mabomu na moshi mweusi unaweza kuonekana karibu na uwanja wa ndege, ulio katikati ya Khartoum na karibu kabisa na makao makuu ya jeshi, huku vifaru vikionekana kwenye baadhi ya mitaa.

Mgonjwa wa kike katika Hospitali ya Al-Zara aliambia BBC siku ya Jumatatu hali ilikuwa mbaya zaidi kwani hakukuwa na dawa wala chakula.Hospitali tayari ina msongamano mkubwa kwani iliwachukua wagonjwa kutoka hospitali nyingine ambayo ilishambuliwa na RSF.

Ukosefu wa vifaa ni tatizo nchini kote, katika hadi majimbo saba, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

"Sasa hospitali nyingi zinaripoti [hazina] vifaa vya matibabu, mifuko ya damu, oksijeni na dawa nyingine muhimu na vifaa vya upasuaji," mwakilishi wa WHO Sudan, Dk Nima Saeed Abid aliambia kipindi cha redio cha Newsday cha BBC.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Volker Perthes ameambia BBC kwamba anawasiliana kila siku na majenerali wawili ambao vikosi vyao vinapigania udhibiti, lakini anasema hawazungumzi.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa saa kadhaa siku ya Jumapili na Jumatatu hayakuzingatiwa kikamilifu.

"Wote wawili walitoa matamshi kwamba vikosi vyao vitajitolea kwa hilo lakini mapatano, au usitishaji, haukuheshimiwa, angalau sio wakati wote na sio katika maeneo yote, lakini tunaenda kuendeleza juhudi hizi," alisema.

Chanzo: Bbc