Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Sudan: Maelfu wakimbia eneo salama la Wad Medani - UN

Mzozo Wa Sudan: Maelfu Wakimbia Eneo Salama La Wad Medani   UN Mzozo wa Sudan: Maelfu wakimbia eneo salama la Wad Medani - UN

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Takribani watu 250,000 wamekimbia mapigano katika mji wa Sudan ambao wakati mmoja unaonekana kama kimbilio salama kwa wale wanaotoroka vita vya wenyewe kwa wenyewe, UN ilisema.

Kikosi cha Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF), ambao wanapigana na jeshi wameingia Wad Madani.

Kwa miezi kadhaa, jiji hilo limehifadhi idadi kubwa ya watu waliokuwa wakitafuta usalama kutokana na mapigano katika mji mkuu, Khartoum.

Watu wa Wad Madani, kusini-mashariki mwa Khartoum, "wanatawanyika pande tofauti", mfanyakazi wa misaada alisema.

"Watu wanakimbia bila kitu zaidi ya nguo mgongoni bila pa kugeukia, pa kwenda," Will Carter, mkurugenzi wa nchi wa Baraza la Wakimbizi la Norway nchini Sudan alikiambia kipindi cha Newsday cha BBC.

Chanzo: Bbc