Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Rwanda na DRC: Vijana zaidi ya 2000 wajiunga na jeshi

Fg9MtTzXgAEgOSK.jpeg Mzozo wa Rwanda na DRC: Vijana zaidi ya 2000 wajiunga na jeshi

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa jeshi la RDC amesema kuwa vijana zaidi ya 200 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametuma maombi ya ujunga na jeshi, kuanzia Jumanne baada ya Rais Felix Tschisekedi kuwataka "wajiunge na jeshi kwa wingi" kwasababu "vita walivyotuingiza majirani zetu vinahitaji kila mtu ajitolee ".

Katika mazungumzo na waandishi wa habari mwishoni mwa juma, Msemaji wa Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (FARDC), Jenerali Sylvain Ekenge, alisema kuwa shughuli ya kuwasajiri vijana jeshini kwa sasa inafayika katika mji mkuu Kinshasa na katika mji wa Goma mashariki mwa nchi.

Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa na Waziri wa habari wa DRCna msemaji wa serikali, Patrick Muyaya.

Jenerali Ekenge alisema: "Zaidi ya 2000 wamejisajiri katika mji wa Goma pekee".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live