Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Libya kupatiwa mwarobaini

Libya Geneva Mzozo wa Libya kupatiwa mwarobaini

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Stephanie Williams Mshauri Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika Masuala ya Libya alisema jana wakati wa kuanza mazungumzo hayo huko Geneva kwamba: viongozi wa Libya sasa wamefikia katika marhala nyeti baada ya kuvuka nje ndefu na ngumu; na kwamba umefika wakati sasa wa kufikiwa mapatano ya kihistoria kwa maslahi ya Libya, wananchi na taasisi za nchi hiyo.

Aguilah Saleh Spika wa Bunge la Libya na Khalid al Mishri Mkuu wa Baraza Kuu la Uongozi la nchi hiyo watakuwa na mazungumzo katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva kuhusu rasimu ya fremu ya katiba kwa ajili ya kuendesha uchaguzi wa Libya.

Awali uchaguzi wa rais na bunge wa Libya ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka jana ili kukamilisha kikamilifu mchakato wa amani uliokuwa ukisimamiwa na Umoja wa Mataifa baada machafuko ya mwaka 2020.

Hata hivyo uchaguzi huo umeakhirishwa kwa muda usiojulikana kutokaa na kushadidi hitilafu kati ya mirengo ya kisiasa na mapigano ya mara kwa mara ya makundi hasimu ya wanamgambo wenye silaha huko Tripoli mji mkuu wa Libya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live