Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzozo wa Israel waripuka Mkutano wa AU

MOZOZO AU Mzozo wa Israel waripuka Mkutano wa AU

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Shtayyeh ameuhimiza Umoja wa Afrika kukifuta kibali cha Israel cha kuwa mjumbe mwenye hadhi ya muangalizi, hatua inayoweka mazingira ya kuzuka mzozo wa ndani.

Hata wakati bara Afrika likikumbwa na msururu wa mapinduzi ya kijeshi na janga la corona, uhusiano na Israel unatarajiwa kuugubika mkutano huo.

Mzozo huo ulianza Julai mwaka jana wakati Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, kukubali kibali cha Israel kuwa na hadhi ya uangalizi kwenye umoja huo, hatua iliyozusha mzozo wa nadra ndani ya jumuiya hiyo ambayo inathamini maelewano.

Wakati wakuu wan chi walikusanyika katika mji mkuu wa Ethiopia Jumamosi, Shtayyeh aliuhimiza umoja huo kupinga hatua ya Faki.

"Israel haipaswi kutuzwa kwa ukiukaji wake na kwa utawala wa kibaguzi inaouwekea watu wa Kipalestina,” amesema.

Mkutano huo huenda ukashuhudia kura ikipigwa ya kuamua kama unaunga mkono au kupinga uamuzi wa Faki, ambao unaweza kusababisha mpasuko usio wa kawaida ndani ya jumuiya hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live