Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzigo wa kodi Kenya kilio kwa watumishi

Kenya Cash Cash Mzigo wa kodi Kenya kilio kwa watumishi

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huku Wakenya wakiendelea kukumbwa na hali ngumu ya maisha kutokana na ongezeko la gharama ya juu ya maisha hakuna matumaini ya afueni kupatikana hivi karibuni .

Hatua hii inajiri baada ya serikali kutangaza kuongeza ada ya Hazina ya kitaifa ya Bima ya afya {NHIF} na Ile ya Hazina ya kitaifa ya Hifadhi ya Jamii {NSSF} .

Viwango vya sasa, ambapo wafanyakazi wanaolipwa hulipa kati ya Sh150 na Sh1,700 kulingana na malipo yao ya kila mwezi, vinaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kiwango kisichobadilika cha asilimia 2.7 ya mshahara wao.

Vilevile kupitia Muswada wa Sheria ya Fedha, kila mfanyakazi atalazimika kulipa asilimia tatu ya mshahara wake ili kuhudumia hazina mpya ya Maendeleo ya Makaazi.Serikali imesisitiza kuwa malipo hayo sio kodi bali ni akiba ingawa makato hayo yatalindwa na sheria na kutolewa kwa mishahara ya wafanyakazi .

Licha ya lalama za wafanyakazi wengi na waajiri kuhusu athari za tozo hiyo ,serikali inasisitiza kwamba mpango huo ni muhimu kwa sababu utaunda nafasi za ajira kwa mamilioni ya watu wasiokuwa na ajira nchini .

Hata hivyo kumekuwa na uhaba wa maelezo sahihi ya jinsi watu watakavyonufaika na miradi hiyo ya nyumba hasa ikizingatiwa kuwa wasiokuwa na kipato hawatochangia ilhali baadhi ya wanaolazimika kuchangia huenda wanalipa madeni ya ujenzi wa nyumba zao binafsi .

Hazina mpya ya maendeleo ya Makazi Akizungumza na waandishi wa habari mapema siku ya Jumatano, katibu wa kudumu katika wizara ya makaazi na maendeleo ya mijini Charles Hinga alisema kwamba ada hiyo itatumika kama hakikisho kwa wawekezaji ambao serikali inataka kujihusisha nao katika ujenzi wa nyumba.

"Baadhi yenu mnauliza kwa nini hatuwezi kutoa fedha hizo kwa hiari? Lakini inapoendeshwa kwa sheria, nikipata bilioni kwa mwezi, ina maana naweza kwenda nje kuwaita wawekezaji na kuwaambia kwamba mradi sheria ipo, nitakusanya fedha baada ya miaka mitatu. ," alisema.

Huku akiifananisha ada hiyo na ushuru wa mafuta unaolipwa na Wakenya, katibu huyo alisema serikali isingeweza kujenga barabara ikiwa haina uhakika wa mtiririko wa pesa kila mwezi kuzipatia kampuni za ujenzi wa barabara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live