Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee wa miaka 84 akiri kumuua mkewe wa miaka 75

Pingu Law Mzee wa miaka 84 akiri kumuua mkewe wa miaka 75

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mzee wa miaka 84 amewashangaza wengi baada ya kukiri kuhusika moja kwa moja katika mauaji ya mkewe mwenye umri wa miaka 75.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Nigeria, polisi katika jimbo la Edo walimzuilia na kumfikisha mahakamani mzee Gabriel Ahuwa ambaye ana taaluma katika udaktrari kwa tuhuma za kumsafirisha jongomeo mkewe kwa panga.

Katika hali isiyo ya kawaida wala ya kutarajiwa, mzee huyo alikiri moja kwa moja kuwa ni yeye alimuuwa mkewe akitaja sababu kwamba mkewe alikuwa anamnyima tendo la ndoa mara kwa mara kama ambavyo mwenyewe alikuwa anataka.

Kulingana na nyaraka ya mashtaka iliyowasilishwa na mashahidi, mshukiwa amekuwa na maswala na mkewe kwa kumpimia haki yake ya ndoa kwa viwango haba.

Mahakama ilielezwa kwamba mtuhumiwa hana majuto na kwamba aliona alichokifanya ndicho suluhisho bora kwa tatizo lake.

Akizungumza na wanahabari, Gabriel alidai mkewe alikuwa amekataa kumpa haki ya ndoa kwa muda mrefu lakini amekuwa akilala na wanaume wengine.

“Mke wangu alikuwa hanisikii, kila nikimuomba aje kulala na mimi huwa anakataa. Tuna watoto saba pamoja, watano wa kiume na wawili wa kike,” alisema.

Alisema alitoa taarifa kwa watoto wake na kwamba binti yake mmoja alikuja kuzungumza na mkewe, lakini hakusikiliza.

“Niliripoti suala hilo kwa familia yangu na familia yake pia lakini alishindwa kuwasikiliza na kuendelea na maisha yake ya zamani na nilikuwa nikisikia habari kuwa wachungaji wanalala naye.

"Kila wakati nilipodai tendo, aidha aliniambia kuwa anaumwa, au alikuwa na kidonda lakini nilikuwa nikisikia fununu kwamba alikuwa akilala na wanaume wengine na sina pesa za kununua tendo la ndoa kutoka kwa vipusa wa kuuza mitaani,"

Alisema kufuatia malalamiko yake, watoto wake walikataa kumtumia pesa pamoja na kupokea simu zake, kwa madai kuwa marehemu mkewe alimtia sumu akilini.

“Kwa hiyo Jumamosi ya wiki iliyopita majira ya alasiri nikiwa ndani ya nyumba, nikachukua panga na kumcharanga mwili mzima. Nilifanya hivyo kwa hasira kwa sababu hakuwa akinitii, na ninataka watu wajue kuhusu hilo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live