Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee ajijengea kaburi na kusherehekea mazishi yake kabla ya kifo chake

9459a54329e2685d Mzee ajijengea kaburi na kusherehekea mazishi yake kabla ya kifo chake

Wed, 19 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Huku bado akiwa hai na buheri wa siha, Chifu Clement Usoro amejiandaa kwa kifo chake

- Mzee huyo mwenye umri wa miaka 73, amejijengea kaburi lake lenye mnara

- Usoro alisema hawataki watoto wake kuandaa hafla ya mazishi baada ya kifo chake

Katika kile wengi wanaweza kuelezea kama jambo lisilokuwa la kawaida, mwanamume Mnigeria Clement Usoro, ameipa maisha na kifo taswira mpya baada ya kujijengea kaburi na hata kusherehekea hafla hiyo kabla ya kuondoka kwake.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 73, katika mahojiano na BBC Pidgin, alisema alifanya maandalizi muhimu ya mazishi yake miaka mitatu iliyopita wakati alitimia umri wa miaka 70.

Kulingana naye, tayari ameandika wosia. Hata hivyo, Usoro, alisema anaendelea kuusahisha kila wakati.

"Nimeandika wosia wangu na nitaendelea kuusahisha kulingana na muda.Nimejenga kaburi langu. Ni kaburi lenye fiti 9 kwa 9. Pia nimejenga mnara kando yake.

"Rafiki yangu alikwenda nami katika duka la jeneza kuona lenye nitapenda.Aliamua kuninunulia. Kama chifu, kuna mambo unatakiwa kufanya kabla ya kufa ama wafanye baada yako," alisema Usoro.

Chifu Usoro pia alifichua kuwa amelipia vitu muhimu vya ibada kwa machifu wake wasaidizi akitoa ng'ombe ili kuwazuia wanawe kuwa na wasiwasi baada ya kifo chake.

Aliongezea kuwa haitaki familia yake kuandaa hafla ya mazishi baada ya kifo chake akidai kuwa kusherehekea kifo chake ni kupoteza muda na pesa.

Mzee huyo pia alisema aliwaagiza watoto wake kumzika siku tatu baada ya kifo chake.

Katika taarifa sawia na hiyo, TUKO.co.ke iliripotia kuwa mwalimu mstaafu mwenye umri wa miaka 94, alitoa jumba lake la kifahari lenye thamani ya KSh 20 milioni kutumika kama nyumba ya wazee katika kaunti ya Nyeri.

Nduhiu Njama aliamua kubadilisha jumba lake la kifahari katika eneo la Tetu ambalo lilijengwa mwaka 1992 baada ya kugundua wazee wengi wanahangaika.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke