Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mwanafunzi wa Zambia aliyeuawa vitani Ukraine, kurejeshwa nyumbani

Lemekhani Nyirenda Lemekhani Nyirenda

Sat, 10 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwili wa mwanafunzi wa Zambia Lemekhani Nyirenda, aliyefariki akipigania Urusi nchini Ukraine, unatarajiwa kurejea nyumbani Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia ametangaza.

Stanley Kakubo aliliambia bunge kwamba mwili huo umefika katika mji wa bandari wa Urusi wa Rostov-on-Don na mwanadiplomasia wa Zambia atafuatana nao kurudi Lusaka, wizara ya mambo ya nje imeandika kwenye Twitter.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 alifariki mwezi Septemba lakini habari za kifo hicho zilitoka mwezi uliopita. Iliiacha familia yake na serikali ya Zambia wakishinikiza mamlaka ya Urusi kupata majibu.

Nyirenda, ambaye alikuwa akisomea uhandisi wa nyuklia huko Moscow, alikuwa akitumikia kifungo kinachohusiana na dawa za kulevya nchini Urusi. Dada yake Muzang'alu Nyirenda alisema amekuwa msafirishaji wa dawa za kulevya bila kujua.

Waziri wa mambo ya nje aliliambia bunge siku ya Ijumaa kwamba serikali ya Urusi ilithibitisha kwamba Nyirenda alisamehewa mwezi Agosti "kujiunga na operesheni ya kijeshi ili kupata msamaha". Bw Kakubo alisema bado anawataka Warusi kutoa maelezo zaidi kuhusu kifo cha kijana huyo raia wa Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live