Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mwanachama wa dhehebu la siri kufukuliwa na kuchunguzwa Kenya

C3d1a303 81cd 41dd Ae62 32e1ade8b293 Mwili wa mwanachama wa dhehebu la siri kufukuliwa na kuchunguzwa Kenya

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: BBC

Familia ya mwanamke wa Uingereza ambaye anadaiwa alifariki baada ya kujiunga na dhehebu moja nchini Kenya imepata haki ya kuufukua mwili wake.

Wakati Lutfunisa Kwandwalla alifariki mwaka wa 2020 katika nyumba ya kiongozi wa kiroho huko Mombasa, maafisa walilaumu "sababu za asili" na hakuna mtu aliyekamatwa.

Lakini familia yake inaamini kuwa aliuawa na wameshinda ombi la mahakama la uchunguzi wa maiti, kwa matumaini ya kuthibitisha hilo."Amri ya mahakama ni ushindi kwa haki’ - kaka yake Imran Admani aliambia BBC."Ilikuwa wakati wa hisia na wakati wa furaha.

"Bi Kwandwalla, 44, alikuwa kutoka Leicester nchini Uingereza na alifika Kenya kama mtalii mnamo Agosti 2019 kutembelea watu wa familia ya mumewe, kaka yake anasema.

Alitarajiwa kurejea Uingereza miezi kadhaa baadaye, lakini vikwazo vya usafiri vya janga la Corona vilimzuia kuondoka Kenya.Wakati huo alijiunga na dhehebu lenye utata katika mji wa pwani wa Mombasa, kulingana na familia yake.Wanadai aliuawa na mwili wake kuzikwa haraka ili kuficha ushahidi.

Kufuatia uamuzi wa wiki jana katika mahakama moja mjini Mombasa, mamlaka ya Kenya sasa lazima ifukue mwili wa Bi Kwandwalla na kufanya uchunguzi wa maiti ili kuthibitisha sababu ya kifo chake.Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na kifo hicho na rekodi za polisi zinaonyesha kuwa kwa sasa hakuna uchunguzi unaoendelea.

Lakini familia ya Bi Kwandwalla iliambia BBC kwamba uchunguzi huo wa maiti ulikuwa hatua ya kwanza ya kuwafanya watamatishe hali ya majonzi.

"Hatua inayofuata ya kubaini kama ilikuwa hila ni kufika kwenye mwili. Tunatumai hivi karibuni tutajua kilichompata," Bw Admani alisema.

Chanzo: BBC