Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mtoto watupwa jalalani

Mwili Wa Mtoto Watupwa Jalalani.png Mwili wa mtoto watupwa jalalani

Mon, 8 May 2023 Chanzo: Radio Jambo

Mwili wa mtoto mchanga wa siku tatu ulitolewa kwenye jalala la Matungulu, Kaunti ya Machakos siku ya Jumapili.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Matungulu Peter Omondi alisema mwili huo ulitolewa kwenye eneo la kutupa taka katika mji wa Tala.

“Mtoto huyo mchanga wa siku tatu alipatikana akiwa ametupwa kwenye eneo la kutupa taka. Mwili huo uliokuwa umeoza kwa sehemu uliondolewa na kupelekwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Kangundo Level 4,” Omondi alisema Jumapili.

Omondi alisema maafisa wa polisi walikimbia katika eneo la tukio baada ya kupokea ripoti kutoka kwa mwananchi

Taarifa hiyo ilitolewa na mwananchi mmoja na kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha Tala.

Alisema maafisa hao walishughulikia eneo la tukio kabla ya mwili kuondolewa.

Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

"Uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea," Omondi alisema.

Chanzo: Radio Jambo