Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mhubiri aliyekuwa ametoweka wapatikana ziwa Victoria

Mwili Wa Mhubiri Aliyekuwa Ametoweka Wapatikana Ziwa Victoria Mwili wa mhubiri aliyekuwa ametoweka wapatikana ziwa Victoria

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: Radio Jambo

Maafisa wa upelelezi wanachunguza kisa ambapo mwili wa mhubiri aliyetoweka ulipatikana katika ufukwe wa Bao, Kombewa kaunti ya Kisumu.

Mwanamume huyo aliyetambulika kwa jina la James Ochola Osewe anaaminika kuwa aidha alifariki kwa kujitoa uhai au alizama katika Ziwa Victoria mnamo Agosti 26 alipoonekana mara ya mwisho.

Mwili wake ulipatikana siku mbili baadaye.

Marehemu alikuwa mhubiri katika Kanisa la Apostolic Church Rare katika kijiji cha Kagwel, polisi walisema.

Mwili huo ulitolewa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti na uchunguzi mwingine, polisi walisema.

Sababu bado haijawekwa wazi.

Wavuvi waliokuwa wakiendesha shughuli zao katika eneo hilo walisema waliigundua mwili ukielea na kuurejesha ufukweni.

Baadaye walipiga simu kwa polisi ambao walitangaza kufungua uchunguzi wa tukio hilo.

Wanakusudia kuhoji wahusika kadhaa katika suala hilo.

Polisi wanasema hawawezi kujua ikiwa aliuawa, alikufa kwa kujitoa uhai au kuzama.

Kwingineko, polisi wanafanya uchunguzi baada ya mwili wa mwanamume uliokuwa umeoza kupatikana katika eneo la Limuru, Kiambu.

Mwili huo uligunduliwa na walinzi katika taasisi hiyo Jumanne mchana.

Maafisa hao walisema mwili huo ulikuwa ndani ya mtambo thabiti karibu na maji taka.

Polisi wanasema mwili huo bado haujatambuliwa na inaonekana kuwa umetupwa humo.

Uchunguzi ulifunguliwa kuhusu mauaji hayo. Mwili huo ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ukisubiri uchunguzi wa maiti na uchunguzi mwingine.

Huko Athi River, Machakos, mwili wa mwanamume ulipatikana kando ya barabara.

Mwili huo ulikuwa na majeraha miguuni, polisi walisema.

Polisi wanasema wanachunguza tukio hilo.

Chanzo: Radio Jambo