Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa jamaa aliyezikwa shuleni wafukuliwa

CRIME SCENE.png Mwili wa jamaa aliyezikwa shuleni wafukuliwa

Fri, 9 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Zoezi la kufukua maiti lililoongozwa na maafisa wa afya lililochukua zaidi ya saa tatu lilifanyika chini ya usalama mkali

- Familia yake ilidai kwamba baba yao alitoa shamba mbadala la kutumiwa kujenga shule ya msingi ya Koroto

- Afisa wa afya wa umma wa Baringo Kaskazini Evans Cherogony alisema kwamba mwili utahifadhiwa kwa muda kabla ya kuzikwa kwenye makaburi ya umma

Familia ya marehemu Paul Kipchabas ambaye alizikwa nje ya darasa katika Shule ya Msingi ya Koroto Day, Baringo Kaskazini hatimaye imefukua mabaki yake.

Zoezi la kufukua maiti lililodumu kwa zaidi ya saa tatu lilifanyika chini ya usalama mkali.

Familia ilikuwa imedai kuwa ardhi ambayo shule hiyo ilijengwa ni yao.

Familia yake ilidai kwamba baba yao alitoa shamba mbadala la kutumiwa kujenga shule ya msingi ya Koroto.

Hata hivyo madai yalikuwa ya muda baada ya hakimu mkazi wa Kabarnet Vienna Amboko kwamba aliamuru mnamo Jumatano, Aprili 7 kaburi la Kipchaba lilichimbwa shukeni humo linawasumbua watoto akili.

Hii ni baada ya familia kuapa kutokubali mwili wa mpendwa wao kufukuliwa.

Afisa wa Afya ya Umma wa Baringo Kaskazini Evans Cherogony aliwaambia waandishi wa habari kwamba mwili utapelekwa katika makafani ya Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Baringo mjini Kabarnet.

Afisa huyo alisema kuwa mwili utahifadhiwa kwa muda kabla ya kuzikwa kwenye makaburi ya umma baada ya familia kukataa kutenga ardhi mbadala kwa mazishi.

Familia ilisema uvamizi ulikuwa umefanywa kwenye ardhi yao na kikundi cha watu wasomi kutoka jamii ya Koroto, inayopatikana katika wadi ya Saimo Soi katika kaunti ya Baringo.

Baada ya mazishi, ambayo yalifanywa usiku, familia waliweka jiwe kubwa halisi juu ya kaburi ili kuzuia majaribio yoyote ya kuutoa mwili.

"Hapo awali tulikuwa tumetoa hekta nyingi kwa shule ya msingi (Koroto) kujengwa. Lakini ile ambayo shule ya sekondari ilijengwa ilikuwa imenyakuliwa. Baba yetu alijaribu kuirudisha ardhi lakini aliugua njiani na baadaye alikufa , " jamaa mmoja wa familia alisema.

Walisema walikuwa wamejiweka tayari kulinda kile walichoamini ni haki yao.

Walitetea mazishi wakisema baba yao, Paul Kipchabas alikuwa amesisitiza mwili wake uzikwe katika shamba hilo atakapoaga dunia.

Mradi wa kujenga shule ya sekondari ulianza mapema mwaka huu. Upinzani mkali ulishuhudiwa kutoka kwa wenyeji wachache, pamoja na familia ya Kipchabas, ambao walidai umiliki wa ardhi chini ya ukoo wao.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke