Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwezi umekamilika ukiwa na malaika mbinguni, mwanahabari Olale amkumbuka mwanawe

Ccbc3b1feaddc3d6 Mwezi umekamilika ukiwa na malaika mbinguni, mwanahabari Olale amkumbuka mwanawe

Tue, 11 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mwanahabari Seth Olale amemkumbuka mwanawe Myles Moses kwa njia ya kipekee ambaye alifariki dunia mwezi mmoja uliopita

- Olale alimpoteza pacha wake mmoja Ijumaa, Aprili 9 akipokea matibabu katika mojawapo ya hospitali humu nchini

- Akitangaza kifo cha mwanawe, Olale alimshukuru Mungu kwa miaka mitatu na miezi minne aliyoweza kuishi naye

Mwanahabari wa runinga ya NTV Seth Olale ameadhimisha mwezi mmoja baada ya kifo cha mmoja wa pacha wake.

Olale alitangaza habari za kifo cha mwanawe kupitia kwenye mitandao ya kijamii ambapo alisema Myles Moses alifariki dunia akipokea matibabu katika hospitali moja humu nchini.

Akimkumbuka mwanawe, haya ndio maneno aliyoyaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, " Mwezi mmoja sasa ukiwa mbinguni ukifurahia na malaika, nakukosa sana mwanangu."

Mashabiki wake mitandaoni walimliwaza kwa kumtumia jumbe za kumtia moyo pia, soma baadhi ya jumbe hizo;

@michael18341," Alisema, " Kila kitu kitakuwa sawa, hebu na mwanao aendele kulala salama."

Verah Okeyo ambaye ni mwanahabari mwenzake alisema," Pole sana kwa kumpoteza mpendwa wako."

Aidha, Olale alimshukuru Mungu kwa miaka mitatu ambayo aliweza kuishi na mwanawe kabla ya mauti kubisha kwenye mlango wake.

"Tutaendelea kukuonyesha mapenzi ya dhati. Asante kwa miaka mitatu na miezi nne tulioweza kukuwa na wewe, ipo siku tutajumuika tena kwa upendo na furaha. Kwaheri ya kuonana baba tunakupenda." Aliandika Seth Olale.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke