Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika alaani utekaji nyara kaskazini mwa Nigeria

Mwenyekiti Wa Umoja Wa Afrika Alaani Utekaji Nyara Kaskazini Mwa Nigeria Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika alaani utekaji nyara kaskazini mwa Nigeria

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Mwenyekiti wa baraza la umoja wa Afrika Moussa Faki Mahammat amelaani mashambulizi yanayozidi kuripotiwa kaskazini mwa Nigeria ambapo Watoto wadogo na kina mama wamelengwa na wapiganaji wa kundi la Boko Haramu kwa kutekwa nyara.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, Faki amewataka ,‘''waliotekeleza uhalifu huo kuwarejesha Watoto waliotekwa mara moja kwa familia zao''.

Ameendelea kusema kwamba, ‘ kitendo hicho ni ishara kwamba tishio la ugaidi na wizi wa mifugo ni masuala yanayotishia sio tu usalama wa eneo la kaskazini mwa Nigeria bali eneo zima na hata mataifa Jirani na jambo ambalo linasikitisha wote barani Afrika.’

Haya yanajiri wakati ambapo wanafunzi 15 walitekwa Jumamosi, katika eneo la Gada, katika jimbo la Sokoto, kaskazini mwa Nigeria.

Mbunge wa eneo hilo aliiambia idhaa ya Hausa ya BBC kwamba shambulizi hilo lilitokea alfajiri, ambapo wapiganaji pia waliwateka wanawake wanne.

Siku ya Alhamisi wiki iiyopita , wanafunzi takriban 300 walitekwa na wapiganaji waliojihami kwa silaha ambao walitumia pikipiki kushambulia shule ya umma katika jimbo la Kaduna.

Aidha, awali makumi ya wanawake waliokuwa kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la Borno, walitekwa huku mamlaka nchini humo ikihofia kwamba huenda wakawa watumwa wa wapiganaji wa kundi hilo wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Jeshi la Nigeria linaongoza vikosi vya usalama katika operesheni ya kusawaka mateka hao waliosemekana kufichwa katika misitu iliyopo kaskazini mwa taifa hilo, huku vifaa kama ndege zisizo na rubani zikitumwa kufanya uchunguzi zaidi katika maeneo yanayojulikana kuwa maficho ya kundi hilo ili kujaribu kuwarejesha Watoto.

Hadi ijumaa, ni Watoto chini ya 70 waliokuwa wameokolewa.

Chanzo: Bbc