Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa BBI Kenya afariki dunia

Screenshot 2021 02 15 At 10.24.22 660x400.png Mwenyekiti wa BBI Kenya afariki dunia

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Seneta wa Garissa nchini Kenya, Mohamed Yusuf Haji(80) amefariki dunia katika hospitali ya Aga Khan, mjini Nairobi ambako alikuwa anapatiwa matibabu, kwa mujibu wa familia yake.

Haji pia alikuwa Mwenyekiti wa Jopo la kazi la Maridhiano nchini Kenya maarufu kama BBI (Building Bridges Initiative).

Haji alijiunga na utawala wa maeneo nchini Kenya mwaka 1960 kama mkuu wa wilaya na kupanda ngazi hadi kuwa miongoni mwa makamishna maarufu mikoani.

Alistaafu uongozi wa utawala wa mikoa mwaka 1998.

Mwaka 2002, aliteuliwa kuwa mbunge na mwaka 2007, akachaguliwa kama mbunge wa eneo la Ijara kwa tiketi ya chama cha Kenya African National Union (KANU).

Wakati wa kifo chake, Haji alikuwa anahudumu muhula wake wa pili kama seneta wa Garissa.

UWEZO WA AJABU, MTU MZIMA ANAYEONGEA SAUTI YA KITOTO “PEPO HILO SHINDWA, WEWE JINI MTOTO”

Chanzo: millardayo.com