Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi Kenya atakiwa kujiuzulu

Chebukati Wafula Chebukati Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi Kenya

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Tume huru ya kusimamia uchaguzi nchini kenya, Wafula Chebukati,Yupo katika wakati mgumu akisubiri maamuzi kutoka Mahakama Kuu kufuatia Ubadhilifu anaohusishwa nao kuufanya waati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2017 wa nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na mmoja wa waombaji waliopeleka Malalamiko Mahakamani hapo, Samwel Clinton Elijah, inaeleza kuwa, uchaguzi huo uligubikwa na mapungufu mengi ikwemo masanduku ya kupigia kura kukutwa yakiwa hayajafunikwa vizuri kama yanavyopaswa kuwa,kitendo kilichopeleka wananchi kukosa imani juu mchakato wa upigaji kura.

"Mshitakiwa(Chebukati)ameshindwa kuitendea haki Katiba na kufuata sheria, tangu kuanzishwa kwa Tume hii haijawah kutokea uchaguzi ka ule, hauna mpangilio, mambo haya yamepelekea kutia dosarai mchakato mzima wa uchaguzi wa Rais uliofanyika Agosti 8,2017, kwa kupata matokeo yaliyogubikwa utata mwingi"amesema Elijah wakati akisoma Waraka uliochapishwa na Mahakama.

Hata hivyo Tume hiyo ipo kwenye maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2022, ikiwa na upungufu wa watumishi wapatao 296 akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live