Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti EAC aendelea na ziara yake ya kikanda

Rais Kusini Sudan Mwenyekiti EAC aendelea na ziara yake ya kikanda

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, hapo jana amezuru nchi ya Angola katika mfululizo wa ziara zake kwenye nchi za Ukanda, akitokea nchini DRC, ambako alikutana na rais Felix Tshisekedi, na kuzungumza kuhusu hali ya usalama mashariki mwa Congo.

Akiwa Kinshasa, rais Kiir, mbali na kutaka kupatikana haraka kwa suluhu ya changamoto ya usalama mashariki mwa DRC na kwenye ukanda, pia alitoa wito wa kufufuliwa kwa mpango wa amani wa Nairobi na Luanda.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na viongozi hao, Kiir alitaka michakato yote miwili kuheshimiwa ili kuhakikisha inatoa suluhu ya kudumu kwa mzozo unaoendelea mashariki mwa DRC.

Kutoka Kinshasa, rais Kiir sasa yuko mjini Luanda, ambako anakutana na rais Joao Laurencio, anayeratibu mazungumzo kati ya rais Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, lengo likiwa kuzungumzia hatua zilizofikia.

Kabla ya kufika Kinshasa, rais Kiir alizuru nchini ya Rwanda na kukutana na rais Kagame, kabla ya kuelekea Rwanda ambako alikutana na rais Evariste Ndayishimiye, ikiwa ni katika juhudi za kusaidia kupata suluhu ya mgogoro unaoendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live