Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti AU azungumza na Putin hali ya chakula Afrika

Senrgal Putinnnn Rais wa Senegal Macky Sall akiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Senegal na mkuu wa Umoja wa Afrika, Macky Sall, amemwambia rais wa Urusi kwamba azingatie athari za uhaba wa chakula kwa bara la Afrika zinaosababishwa na mzozo wa Ukraine, shirika la habari la AFP limeripoti.

Marais hao wawili wamekutana katika mji wa kusini mwa Urusi wa Sochi. AFP inamnukuu Rais Sall akisema kwamba Rais Vladimir Putin atalazimika "kufahamu kwamba nchi zetu, hata kama ziko mbali na mzozo huo, pia ni waathirika katika ngazi ya uchumi" kutokana na mzozo huo.

Aliongeza kuwa umuhimu wa chakula unapaswa kuwa "nje" ya vikwazo vya Magharibi kwa Urusi. Kabla ya mzozo huo, zaidi ya 40% ya ngano inayotumiwa barani Afrika ilitoka Ukraine au Urusi.

Kabla ya kuondoka Senegal, ofisi ya rais Sall ilisema ziara hiyo ililenga kukomboa akiba ya nafaka na mbolea ambayo kwa sasa imezuiwa katika bandari za Ukraine.

Nchi za Afrika zinaathirika haswa kutokana na kupanda kwa bei kunakosababishwa na vita Hapo awali, shirika la habari la Reuters lilinukuu Kremlin ikisema kwamba Putin atatoa maelezo "ya kina" kuhusu kile kinachotokea kwa nafaka ya Ukraine.

Katika hotuba yake kwa umma baada ya mkutano huo, iliyonukuliwa na AFP, Putin alisema Urusi "siku zote iko upande wa Afrika".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live