Serikali ya Somalia imetangaza kuwa mwanzilishi mwenza na mwanamgambo mkuu wa al-Shabab, Abdullahi Nadir, aliuawa tarehe 1 Oktoba katika eneo la kusini la Jubba ya Kati. Wizara ya habari ya Somalia ilisema kuwa Nadir alikuwa mkuu wa kitengo cha uenezaji wa kidini cha al-Shabab na alikuwa akisakwa na mtu ambaye akifanikisha kukamatwa kwake agepewa kiasi cha $3m za Marekani.
Iliongeza kuwa al-Shabab walimchukulia Nadir kama mrithi anayetarajiwa wa kiongozi wake wa sasa, Ahmed Omar Diriye, almaarufu Abu Ubaidah, ambaye kwa muda mrefu imekuwa ikisemekana kuwa yupo "katika afya mbaya".
Vyombo vya habari vya kibinafsi viliripoti kwamba Nadir aliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani. Wizara ya habari ilisema kuwa vikosi vya usalama vya Somalia na washirika wa kimataifa walimuua Nadir katika operesheni ya pamoja, lakini haikutaja shambulio la ndege zisizo na rubani