Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi wa Habari Rwanda atupwa jela miaka mitatu

Asgdf Mwandishi wa habari Jean Paul Nkundineza

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Rwanda imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu Gerezani Mwandishi wa habari Jean Paul Nkundineza baada ya kukutwa na hatia ya utumiaji wa maneno yasiyo stahiki kwenye mitandao ya kijamii.

Mbali ya hukumu hiyo amepigwa faini ya Milioni Moja na laki moja faranga ya Rwanda.

Mwandishi huyo amekutwa na hatia ya kutoa maneno yasiyokuwa na staha kwa Miss Rwanda mwaka wa 2016 Jolly Mutesi kupitia mtandao wa kijamii wa Youtube.

Kwa upande wa wakili wake Jean Paul Ibambe amefahamisha kuwa hakuna makosa aliyoyafanya bali alifanya kazi yake ya uandishi wa habari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live