Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi wa Habari Bi Sandra ahamishiwa Gereza Kuu Bujumbura

Sandra Muhoza  Scaled Mwandishi wa habari wa tovuti ya La Nova Bi. Sandra Muhoza

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwandishi wa habari wa tovuti ya La Nova Bi. Sandra Muhoza amehamishiwa katika Gereza Kuu la Mpimba mjini Bujumbura baada ya kumaliza siku kadhaa katika Gereza la ujasusi.

Muhoza alikamatwa siku ya Jumamosi iliyopita mkoani Ngozi Kaskazini mwa Burundi akishutumiwa kusambaza ujumbe ambao hauna staha katika mtandao wa kijamii wa Whatsapp.

Umoja wa waandishi wa habari nchini Burundi umeitaka Mamlaka kumwachilia huru mwandishi huyo bila kikwazo chochote.

Mkurugenzi wa tovuti ya La Nova, Pascal Ndayisenga amesema kukamtwa kwa Sandra Muhoza haikufuatwa sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live