Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwandishi ashikiliwa na Idara ya Ujasusi Burundi

Sandra Muhoza  Scaled Sandra Muhoza

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa kutoka Bujumbura zinasema kuwa Mwandishi wa habari wa Burundi amezuiliwa tangu Jumapili na Idara za Ujasusi Mjini Bujumbura na kuibua wasiwasi kuhusu uhuru wa vyombo vya habari katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Sandra Muhoza, 42, ni Mwandishi wa habari wa La Nova Burundi, chombo cha habari cha mtandaoni kinachojulikana kuwa karibu na Mamlaka.

Mumewe alipokea Jumapili ujumbe kutoka kwa simu yake ukisema ‘mkeo anazuiliwa katika Makao Makuu ya Idara ya Kitaifa ya Ujasusi.

Hii si mara ya kwanza kwa wanahabari kulengwa nchini Burundi. Mnamo Mei 2023, Mwanahabari Floriane Irangabiye alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kudhoofisha usalama wa nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live