Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanawe wa kupanga wa Mike Sonko, Gift Osinya afuzu katika mtihani wa KCSE

Cb561b0b63955196 Mwanawe wa kupanga wa Mike Sonko, Gift Osinya afuzu katika mtihani wa KCSE

Tue, 11 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko amelelezea furaha yake mitandaoni baada ya mwanawe wa kupanga Gift Osinya kuibuka miongoni mwa watahiniwa bora katika mtihani wa KCSE mwaka wa 2020.

Familia ya Sonko ilitangaza kwamba Gift Osinya alipata gredi ya B- pindi ya matokeo yalipotolewa na Waziri wa Elimu Fred Matiang'i.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Sonko alikuwa na haya ya kusema." Baada ya kupata alama ya 399 katika mtihani wa KCPE, Gift Osinya alijiunga na shule ya upili ya Lenana ambapo pia ametufurahisha miaka minne baada ya kupata gredi ya B- katika mtihani wake wa kitaifa wa KCSE," Sonko alisema.

Gift na kakake mdogo waliunganishwa na familia ya Sonko mwaka wa 2014 baada ya mama yao kuuawa kwenye shambulizi la kigaidi akiwa kanisani mjini Mombasa.

Sonko amekuwa akiwalea wawili hao tangu kifo cha mama yao, amewapa elimu na kuhakikisha wana malezi bora.

" Wakati magaidi walishambulia kanisa moja mjini Likoni siku ya Jumapili, Machi 23, 2014, mamake Gift alipoteza maisha yake pamoja na waumini wengine. Kakake gift aliachwa na risasi kichwani mwake hali ambayo ilimuacha Gift na wasiwasi mkubwa lakini tunashukuru Mungu kwa kuwaponya," Sonko alisema.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke