Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaume mwenye miaka 54 arejea shule ya msingi

FB IMG 1664725488294 Mwanaume mwenye miaka 54 arejea shule ya msingi

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 54 aliyefahamika kwa jina moja la Rusengamihigo kutoka nchini Rwanda, ameamua kuisaka elimu na kurejea darasani.

Mwanaume huyo amewashangaza wengi baada ya kuanza elimu ya msingi (Primary School) akiwa tayari ni mtu mzima.

Rusengamihigo alipokwenda Shuleni hapo kwa ajili ya usajili, yeye alipenda kuanzia darasa la tatu (3) ila Waalimu wa shule hiyo wakapendelea na kumshauri aanzie daraja la tano (5).

Baba huyo tayari ameanza shule licha ya changamoto anazokabiliana nazo akiwa na sare za shule pamoja na Wanafunzi wenzie kumshangaa kutokana na umri wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live