Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaume auawa kwa tuhuma za kuiba mkate

Mwanaume Auawa Kwa Tuhuma Za Kuiba Mkate Mwanaume auawa kwa tuhuma za kuiba mkate

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Imegundulika kuwa mwanaume mmoja aliyedungwa kisu na umati wa vijana wengine hadi akafa, kwa tuhuma za kuiba mkate nchini Nigeria, alikuwa na matatizo ya kiakili.

Hii ilithibitishwa na baadhi ya jamaa na majirani wa Ebimotimi Freeborn Opuofoni.

BBC iligundua kuwa haukuwa hata mkate ulioibiwa, bali ilikuwa ni Madiga kulli, aina ya chakula cha unga kinacholiwa katika sehemu ya jimbo la Bayelsa nchini Nigeria.

Madiga ni chakula kinachotengenezwa na waoka mikate wa kienyeji ambacho ni sawa na mkate, lakini ni huwa na ugumu zaidi na watoto na watu wazima huula na siagi au bila kikavu.

Madiga ni chakula kinachofanana na mkate ambacho Ebimotimi Freeborn alishutumiwa kuibaImage caption: Madiga ni chakula kinachofanana na mkate ambacho Ebimotimi Freeborn alishutumiwa kuiba Ndugu wa karibu wa familia yake, Kenneth Amewuga alisema Freeborn alikuwa na bidii na alihitimu chuo kikuu na matokeo mazuri sana.

Alisema hatahivyo kuwa “marehemu alifahamika mtaani kwake kuwa ni mgonjwa wa akili, ambapo wakati mwingine huwanyang’anya watu simu, si kwa ajili ya kuziuza bali kuzitupa barabarani au kuziharibu”.

Aliongeza kuwa “tabia yake ilimfanya baba yake kuwa na wasiwasi, kabla ya kifo cha chake miaka michache iliyopita.

Tukio hilo liligusa moyo wangu'

Kifo cha Freeborn kilikuwa msiba mkubwa kwa familia yake, ambao waliomboleza msiba wake.

Mmoja wa ndugu zake, Beauty Edisemi Opufoni, aliambia BBC huku akitokwa na machozi kwamba kifo cha kaka yake kiliwasikitisha na kumuacha katika hali ya mshangao, kwa sababu hakuwahi kumletea kifo hapo awali.

Alisema ingawa kaka yake alitumia miaka mitatu hadi minne baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, Mungu hakukusudia apate kazi.

Jeshi la polisi mjini Bayelsa linasema kuwa limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mtu huyo mwenye umri wa miaka 32.

Msemaji wa Polisi wa Bayelsa, SP Asinim Butswat, alitoa taarifa kwamba watu waliokamatwa ni miongoni mwa majambazi waliompiga vijana.

Chanzo: Bbc